• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa UM awapongeza waasi wa Yemen kuacha mashambulizi ya makombora

    (GMT+08:00) 2018-11-20 09:44:55
    Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia suala la Yemen Bw. Martin Griffiths, amelipongeza kundi la waasi wa Houthi kuacha mashambulizi ya makombora dhidi ya Saudi Arabia.

    Bw. Griffiths pia ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa ana nia ya kuzishawishi pande hizo mbili zinazopambana kufanya mkutano nchini Sweden. Amesema amepata uhakikisho kutoka kwa viongozi wa makundi hayo kushiriki kwenye mkutano huo.

    Habari pia zinasema ndege za jeshi la muungano linaloongozwa na Saudi Arabia zimefanya mashambulizi 12 dhidi ya vituo vya waasi wa Houthi mjini Hodeidah, Yemen.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako