• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pande hasimu Sudan Kusini zakubaliana kusitisha vita kaskazini mwa nchi

    (GMT+08:00) 2018-11-20 09:45:18

    Kikosi cha ulinzi cha Sudan Kusini SSDF na kundi hasimu la makamu rais wa zamani Riek Machar wamekubaliana kusimamisha vita katika jimbo la Wau kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

    Msemaji wa kundi la SPLA-IO Bw. Lam Paul Gabriel amesema, kundi lake limekubaliana na majeshi ya serikali ya Sudan kusimamisha vita ili kudumisha usalama na kuwawezesha wakulima kuvuna mazao yao kabla ya msimu kiangazi.

    Habari zinasema pande hizo mbili pia zimekubaliana kusitisha mapambano katika jimbo la Mto Yei na kufungua njia kwa ajili ya misaada ya kibinadamu katika eneo la Pibor.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako