• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China awasili mjini Manila, Philippines

    (GMT+08:00) 2018-11-20 12:36:35

    Rais Xi Jinping wa China amewasili mjini Manila na kuanza ziara ya kiserikali nchini Philippines.

    Rais Xi amesema, tangu rais Rodrigo Duterte aingie madarakani, ushirikiano kati ya nchi hizo mbili umefungua ukurasa mpya, kuwaletea watu wa nchi hizo mbili manufaa halisi, na kutoa mchango mkubwa katika amani, utulivu na ustawi wa kikanda. Rais Xi pia amesema, Philippines na China zikiwa nchi jirani na makundi mapya ya kiuchumi, kuendeleza urafiki kati yao ni chaguo pekee sahihi.

    Katika ziara hiyo, rais Xi anatarajia kubadilishana maoni na viongozi wa Philippines katika kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili na masuala yanayofuatiliwa zaidi ya kimataifa na ya kikanda. Amesma ana imani kuwa, ziara hiyo itaimarisha urafiki wa jadi kati yao, na kuongeza ushirikiano wa kunufanishana ili kutimiza malengo ya maendeleo ya pamoja na kunufaisha watu wa nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako