• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China awasili mjini Manila,Philippines

    (GMT+08:00) 2018-11-20 14:46:02

    Rais Xi Jinping wa China amewasili mjini Manila na kuanza ziara ya kitaifa nchini Philippines.

    Kwa niaba ya watu na serikali ya China, rais Xi ametoa salamu ya nia dhati kwa watu na serikali ya Philippines. Amesema, tangu rais Rodrigo Duterte kushika zamu, ushirikiano kati ya nchi hizo mbili umefungua mlango upya, kuwaletea watu wa nchi hizo mbili manufaa halisi na kutoa mchango mkubwa katika amani, utulivu na ustawi wa kikanda. Rais Xi pia amesema, Philippines na China zikiwa nchi jirani na makundi mapya ya kiuchumi, kuendeleza urafiki kati yao ni njia pekee sahihi.

    Katika ziara hiyo, rais Xi anatarajia kubadilishana maoni na viongozi wa Philippines kaitka kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili na masuala yanayofuatilia zaidi ya kimataifa na ya kikanda. ana imani kuwa, ziara hiyo itaimarisha urafaiki wa jadi kati yao, kuongeza ushirikiano wa kunufanishana ili kutimiza malengo ya maendeleo ya pamoja na kunufaisha watu wa nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako