• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea Kusini yasema Korea Kaskazini inatakiwa kushirikiana na jamii ya kimataifa kwa maendeleo ya kiuchumi

    (GMT+08:00) 2018-11-20 20:01:48

    Waziri wa muungano wa Korea Kusini Cho Myoung-gyon amesema, Korea Kaskazini inahitaji kushirikiana na jamii ya kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi.

    Cho amesema, ni lazima kwa Korea Kaskazini kushirikiana na jamii ya kimataifa kwa maendeleo ya kiuchumi ambayo nchi hiyo inataka kutimiza, na kuongeza kuwa, bila ya kupata maendeleo katika mchakato wa kumaliza silaha za nyuklia, Korea Kaskazini haitaweza kutimiza malengo yake. Pia amesema, kama utulivu wa kudumu utapatikana katika Peninsula ya Korea, mlango mpya utafunguliwa kwa Korea Kaskazini.

    Wakati huohuo, wizara ya ulinzi ya Korea Kusini imesema, Korea Kaskazini imeharibu vituo 10 vya ulinzi ndani ya Ukanda Usio na Majeshi (DMZ), kama ilivyokubaliwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako