• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Ufaransa zaapa kuzidisha ushirikiano wa mazingira ya kiikolojia

    (GMT+08:00) 2018-11-20 18:47:02

    Naibu waziri mkuu wa China Bw. Han Zheng amekutana na waziri wa ikolojia wa Ufaransa Bw. Francois de Rugy, ambapo wamezitaka pande hizo mbili kuimarisha ushirikiano katika maeneo kadhaa ikiwemo ulinzi wa mazingira ya kiikolojia.

    Bw. Han amesema, China iko tayari kushirikiana na Ufaransa kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na marais wa nchi hizo mbili na kuinua uhusiano kati ya pande mbili ufikie kiwango cha juu zaidi. Pia amesema, China inatilia maanani katika ushirikiano wa kimataifa kuhusu mazingira ya kiikolojia, huku ikitaka kuimarisha mazungumzo na mawasiliano na upande wa Ufaransa katika sekta za ulinzi wa mazingira ya kiikolojia, mabadiliko ya hali ya hewa, hifadhi ya wanyamapori ili kufanya juhudi za kujenga dunia yenye usafi na uzuri.

    Bw. De Rugy amesema, Ufaransa inathamini ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, na inataka kuzidisha ushirikiano huo na China katika sekta mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako