• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Bei ya nyanya yapanda

    (GMT+08:00) 2018-11-20 19:06:33

    Taifa likijiandaa kukaribisha msimu wa Krismasi 2018, bei ya nyanya imeanza kupanda. Uchunguzi wa vyombo vya habari umebainisha maeneo mengi nchini yameanza kushuhudia ongezeko la bei ya kiungo hiki cha mapishi.

    Masoko mengi katika maeneo ya, Murang'a, Thika, Ruiru, Zimmerman, Githurai na Mwiki, kifungu cha nyanya tatu za ukubwa wa wastani kinauzwa Sh20, huku moja kubwa ikigharimu kati ya Sh10-20.

    Mwezi Aprili hadi Oktoba masoko yalisheheni nyanya kutokana na mvua iliyoshuhudiwa kipindi hicho, hali iliyosababisha bei yake kushuka.

    Msimu huo Sh20 zingenunua kati ya nyanya nne hadi sita. Wakulima wanasema ukosefu wa bidhaa hii umechangiwa na jua kali ambalo linashuhudiwa maeneo mengi nchini. Kreti moja ya nyanya inauzwa shilingi kati ya shilingi 5000-6000. Licha ya ukosefu wa nyanya, wakulima wa zao hili wanasema kuwa wahangaishwa sana na mawakala, ambao wamekuwa changamoto kuu kwa kilimo chao. Wanasema kwamba mawakala huwapunja kwa kuamua bei ya mazao yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako