• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Mazao ya mahindi yapanda kwa asilimia 20.

    (GMT+08:00) 2018-11-20 19:06:53

    Wakenya hawana hofu ya unga wa ugali hadi mwezi Juni mwaka uajo. Hii ni kwa sababu mavuno ya mahindi ya mwaka huu yameongezeka kwa asilimia 20 kutoka msimu uliopita. Mwaka huu, zaidi ya magunia milioni 41 ya kilo tisini ya mahindi yalivunwa. Hata hivyo, wakulima huenda wakauza mazao yao kwa bei ya chini kwa sababu ya wingi wa mahindi, huku bei ya unga ikitarajiwa kupungua. Mwaka uliopita, magunia milioni 34 ya mahindi yalivunwa, kinyume na miaka ya hapo awali ambapo mavuno yalikuwa duni. Hali hii ililazimu serikali kununua mahindi kutoka mataifa mengine ili kukabiliana na mfumuko wa bei ya unga wa ugali. Mwaka uliopita, Kenya ilinunua mahindi yenye thamani ya shilingi bilioni 40.2, hii ikiwa ni juu mno kutoka shilingi bilioni 3.6 mwaka wa 2016. Ukosefu wa mahindi mwaka jana ulisababisha bei ya pakiti ya kilo mbili ya unga wa ugali kuuzwa kwa shilingi 153. Baada ya mahindi kuagizwa kutoka nje, pakiti ya kilo mbili ikauzwa kwa shilingi 90.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako