• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito tamaduni tofauti kuishi kwa masikilizano

    (GMT+08:00) 2018-11-20 19:14:45

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuunda mazingira kwa watu wenye tamaduni na hadhi tofauti kuishi pamoja kwa masikilizano na kuepusha ubaguzi na ukandamizaji.

    Bw. Guterres amesema hayo kwenye ufunguzi wa Baraza la 8 la Muungano wa Ustaarabu wa dunia wa Umoja wa Mataifa UNAOC. Amewahimiza watu kutoa tahadhari kwa makundi mapya ya Nazi na yanayopinga Uyahudi, na kuwaonya watu kuacha ubaguzi na unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto wa kike.

    Aidha Bw. Guterres amesisitiza kuwa jitihada zinapaswa kufanywa ili kujenga jamii inayoheshimu na kufuatilia maslahi ya watu wote na kusisitiza kuinua uwezo wa uvumbuzi na uhai wa vijana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako