• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kundi la Taliban lafanya mazungumzo na Marekani kuhusu kuanzisha mchakato wa amani nchini Afghanistan

    (GMT+08:00) 2018-11-20 19:15:12

    Kundi la Taliban la Afghanistan na Marekani zimefanya mazungumzo ya mwanzo kuhusu kuanzisha mazungumzo ya amani huko Doha, nchini Qatar, lakini hakuna makubaliano yaliyofikiwa.

    Msemaji wa kundi hilo Bw. Zabihullah Majahid amesema, mazungumzo hayo yanalenga kufanya maandalizi kwa mazungumzo ya amani, lakini hayakufikia makubaliano. Viongozi wa Taliban wamekataa muda wa mwisho uliowekwa na Marekani kwa mazungumzo ya amani.

    Ubalozi wa Marekani huko Kabul haujatoa kauli yoyote kuhusu mazungumzo hayo, huku mjumbe maalum wa Marekani anayeshughulikia suala la Afghanistan Bw. Zalmay Khalilzad akisema anatarajia kufikia makubaliano ya amani na Taliban mnamo tarehe 20 mwezi Aprili mwaka ujao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako