• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Palestina wapongezana juu ya maadhimisho ya miaka 30 tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi

    (GMT+08:00) 2018-11-20 19:44:05

    Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Palestina Bw. Mahmoud Abbas wamebadilishana salamu za pongezi katika kusherehekea miaka 30 tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi.

    Rais Xi amesema, historia ya urafiki kati ya China na Palestina ni ndefu, na China ni moja kati ya nchi zinazounga mkono haki ya watu wa Palestina, na pia ni moja kati ya nchi zilizotambua mapema kundi la PLO la nchi hiyo. Amesema China itaendelea kuhimiza mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel na kuendelea kutoa mchango katika kutimiza utatuzi wa haki na wa pande zote wa suala la Palestina mapema iwezekanavyo.

    Rais Abbas amesema, anaona fahari juu ya urafiki wa jadi kati ya nchi hizo mbili na watu wake, huku akisifu mchango muhimu uliotolewa na China katika kuunga mkono watu wa Palestina na shughuli yake. Amesema ataendelea kutilia maanani na kuhimiza maendeleo ya uhusiano huo, ili kuwanufaisha watu wa nchi hizo mbili na kutimia mustakabali wa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako