• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Philippines wafanya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2018-11-20 21:20:52

    Rais Xi Jinping wa China na mwenzake Rodrigo Duterte wa Philippines wamefanya mazungumko huko Manila.

    Marais hao wamepanga maendeleo ya uhusiano wa pande mbili, kufikia maoni muhimu ya pamoja ya kujenga uhusiano na ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbili kwenye msingi wa kuheshimiana, kutendeana kwa dhati, kunufaishana kwa usawa, kushirikiana na kupata mafanikio ya pamoja.

    Rais Duterte ametoa pongezi kwa mafanikio yaliyopatikana China katika miaka 40 iliyopita tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango.

    Naye rais Xi Jinping amesisitiza kuwa, kujenga uhusiano na ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kunaendana na matarajio ya watu wa China na Philippines na mahitaji ya maendeleo ya uhusiano wa pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako