• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Uhispania na Morocco wataka kuwa wenyeji wa kombe la dunia mwaka 2030

    (GMT+08:00) 2018-11-21 09:07:33
    Nchi ya Uhispania imeandikia barua Morocco, kuomba ushirikiano pamoja na Ureno ili kuomba kwa pamoja kuwa wenyeji wa michuano ya kombe la dunia mnamo mwaka 2030.

    Ombi hilo, limetolewa na waziri mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez wakati akiwa ziarani nchini Morocco mwanzoni mwa wiki hii.

    Uhispania imewahi kuwa mwenyeji wa kombe la dunia mara moja, mwaka 1982.

    Morocco imejaribu kuomba kuwa mwenyeji wa Kombe la dunia la mwaka 1994, 1998, 2006, 2010 na 2026 bila mafanikio

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako