• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RIADHA: Mwanariadha wa Uganda aweka rekodi mpya ya dunia mbio za kilomita 15

  (GMT+08:00) 2018-11-21 09:08:37

  Mwanariadha Joshua Cheptegei wa Uganda amevunja rekodi ya dunia ya mbio za kilomita 15 ambayo ilishikiliwa na Mkenya Leonard Komon kwa miaka minane baada ya kutimka mbio za Zevenheuvelenloop mjini Nijmegen nchini Uholanzi kwa dakika 41:05.

  Cheptegei alifuatiwa kwa karibu na raia wa Eritrea Abrar Osman (42:34), raia wa Ethiopia Muktar Edris (42:55) na Mjerumani Richard Ringer (43:39) katika mbio hizo.

  Uganda pia ilinyakua taji la wanawake kupitia kwa Stella Chesang (47:19) ambaye alifuatiwa sekunde chache baadaye na Mkenya Evaline Chirchir (47:35) na Mholanzi Susan Krumins (47:41).

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako