• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wasema sera za elimu shirikishi kwa wakimbizi ni muhimu kwa maendeleo ya Afrika

    (GMT+08:00) 2018-11-21 09:14:15

    Serikali za nchi za Afrika zimehimizwa kuweka sera za elimu kwa ajili ya watoto na vijana waliokimbia migogoro na majanga ili kuchochea ukuaji, amani na utulivu barani humo.

    Wakiongea kwenye uzinduzi wa ripoti kuhusu usimamizi wa elimu duniani GEM kwa mwaka 2019 iliyotolewa na Shirika la elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa mataifa UNESCO, wataalamu wamesema sera zinazohimiza elimu kwa watoto na vijana wakimbizi, zinahitajika kuhakikisha wanashirikishwa kwenye maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nchi zao.

    Mshauri mwandamizi wa Jumuiya ya ushirikiano wa kiserikali wa nchi za mashariki na pembe ya Afrika IGAD Bw. Kebede Tsegaye amesisitiza haja ya nchi za Afrika kuhusisha elimu ya wakimbizi kwenye mipango ya maendeleo ya taifa.

    Ripoti hiyo ya UNESCO inasema elimu inaweza kuwa nyenzo ya kuhimiza masikilizano kati ya makabila ambayo ni muhimu katika kuzuia migogoro inyosababisha msukosuko wa wakimbizi barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako