• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya dunia yasema GDP ya Uganda imekua kwa asilimia 6.1 mwaka huu

    (GMT+08:00) 2018-11-21 09:14:37

    Benki ya dunia imesema Pato la ndani GDP la Uganda limeongezeka hadi kufikia asilimia 6.1 katika mwaka wa fedha 2017/18, kutoka asilimia 3.9 ya mwaka wa fedha uliopita. Benki hiyo kwenye ripoti yake ya 12 kuhusu uchumi wa Uganda imesema ufufukaji huo ni mkubwa zaidi kuliko asilimia 5.5 iliyokadiriwa kwenye ripoti iliyopita iliyotolewa mwezi Mei mwaka huu.

    Ripoti inasema kufufuka huko kunatokana na kufufuka kwa uzalishaji wa nafaka na kuongezeka ghalfa kwa mikopo kwenye sekta binafsi katika nusu ya pili ya mwaka wa fedha uliopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako