• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Ufilipino zaanzisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote

    (GMT+08:00) 2018-11-21 09:14:58

    Rais Xi Jinping wa China ambaye yuko ziarani nchini Ufilipino jana alifanya mazungumzo na mwenzake Rodrigo Duterte, na kuamua kuanzisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote.

    Hii ni mara ya kwanza kwa rais wa China kufanya ziara nchini Ufilipino katika miaka 13 iliyopita tangu mwaka 2005 serikali ya awamu iliyopita ya Ufilipino kuwasilisha mahakamani kesi ya usuluhishi kuhusu mamlaka ya bahari ya Kusini ya China.

    Mwaka 2016 baada ya rais Rodrigo Duterte kuingia madarakani, China na Ufilipino zilirejea kwenye njia sahihi ya kutatua suala la bahari ya kusini ya China kupitia mazungumzo. Tangu hapo rais Xi Jinping wa China amekutana na Bw. Duterte mara sita, na kufungua ukurasa mpya wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Rais Duterte amesema ziara ya rais Xi wa China nchini Ufilipino ina umuhimu wa kihistoria, na pia ni hatua muhimu kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Amesisitiza kuwa Ufilipino inakubali kwamba nchi za kikanda zitalinda kwa pamoja amani na utulivu wa bahari ya kusini ya China, na China imechukua msimamo sahihi wakati wa kushughulikia mambo ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako