• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chama tawala cha Msumbiji chataka upinzani waache tishio la vita

    (GMT+08:00) 2018-11-21 09:26:12

    Msemaji wa chama tawala cha Msumbiji FRELIMO Bw. Caifadine Manasse, amekitaka chama cha upinzani cha nchi hiyo RENAMO kuacha tishio dhidi ya mchakato wa amani, hasa kutokana na kuwa Rais wa nchi hiyo Filipe Nyusi anafanya juhudi kufanikisha mchakato huo.

    Msemaji huyo amesema hayo kufuatia kauli iliyotolewa na Kiongozi wa mpito wa RENAMO Bw. Ossufo Momade, aliyesema kwenye mkutano wa njia ya video kuwa kama mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa unaodhaniwa kuwa na dosari za ufisadi hautapitiwa upya, ataanzisha mapambano ya kisilaha. Hata hivyo Bw. Manasse amesema RENAMO inatakiwa kuzingatia maendeleo ya nchi, jambo ambalo Rais na wananchi wanalitaka.

    Jumatano iliyopita baraza la Katiba liliidhinisha matokeo ya chaguzi kwenye manispaa 52 kati ya 53, lakini RENAMO imesema kulikuwa na ufisadi kwenye manispaa zote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako