• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Kusini kufuta hitaji la uzoefu kwenye ombi la ajira kwa kazi za serikali

    (GMT+08:00) 2018-11-21 09:26:31

    Mpango wa serikali ya Afrika Kusini kufuta hitaji la uzoefu kwa waombaji wa mara ya kwanza wa kazi za utumishi wa umma, umekaribishwa na watu wa Afrika Kusini. Mhadhiri wa chuo Kikuu cha Witwatersrand Profesa Jannie Rossouw, amesema jaribio lolote la kupunguza hali ya vijana kutokuwa na ajira linakaribishwa, lakini ubora wa huduma hautakiwi kuathiriwa.

    Waziri wa utumishi wa umma na utawala Bibi Ayanda Dlodlo, jumatatu alitangaza kuwa kuanzia mwezi Aprili mwakani, wahitimu wote waombaji wa nafasi za ajira serikalini, hawatatakiwa kuwa na uzoefu kabla ya kuomba nafasi.

    Bibi Dlodlo amesema hatua hiyo ya serikali haitaathiri ubora wa huduma, kwa kuwa kutakuwa na mahitaji ya kitaaluma na kiufundi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako