• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yafunga bureau de change mkoani Arusha kutokana na tuhuma za utakatishaji fedha

    (GMT+08:00) 2018-11-21 09:41:46

    Benki kuu ya Tanzania BOT imesema imefunga bureau de change katika Mkoa wa Arusha, kaskazini mwa nchi hiyo, kutokana na tuhuma za utakatishaji fedha.

    Gavana wa BOT Bw. Florens Luoga amesema uchunguzi wa idara mbalimbali za serikali unatekelezwa na watu wanaohusiana na fedha haramu watashitakiwa.

    Ameongeza kuwa, kufunga bureau de change ni sehemu ya juhudi za kupambana na watakatishaji fedha na watu wasio na leseni wanaojihusisha na shughuli za kubadilisha fedha kote nchini.

    Pia amesema benki kuu ya Tanzania imesimamisha utoaji wa leseni ya shughuli za kubadilisha fedha na itaanza kutoa leseni baada ya kanuni mpya kuanza kutekelezwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako