• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu wenye silaha wamteka nyara raia wa Italia mkoa wa pwani nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2018-11-21 17:45:49

    Watu wasiofahamika waliokuwa na silaha wamevamia kituo cha kulelea watoto yatima katika mji wa pwani wa Malindi, nchini Kenya na kumteka nyara mwanamke mmoja raia wa Italia na kujeruhi watu wengine watano.

    Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Kenya Joseph Boinet amesema, watu hao waliokuwa na bunduki aina ya AK47 walivamia kituo cha Chakama kilichoko umbali mfupi kutoka mji wa Malindi, kaunti ya Kilifi jana jioni. Amesema polisi wamesambazwa ili kuwasaka watuhumiwa hao, na kutaka umma katika eneo hilo kutoa taarifa mara moja polisi kama wakiwaona watuhumiwa hao na mateka wao.

    Kenya inawalaumu wapiganaji wa kundi la Al Shabaab la Somalia kwa mfululizo wa utekaji nyara wa raia wa kigeni na mashambulizi ya kutumia maguruneti na mabomu ya kutega ardhini katika eneo lake la mpakani na Somalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako