• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yatuma ombi la kujiunga na Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo,OECD.

    (GMT+08:00) 2018-11-21 19:50:12

    Rwanda imetuma ombi la kujiunga na Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo-OECD .

    Haya yalithibitishwa jana na Waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Dkt Richard Sezibera kwenye kikao chake cha kwanza na wanahabari tangu achukue nagfasi hiyo ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Louise Mushikiwabo ambaye sasa amechaguliwa kama Katibu Mkuu wa Francophonie.

    OECD ni jukwaa la nchi 36,nyingi yazo nchi zilizoendelea,ambazo zinashirikiana kwa ukaribu ili kuinua uchumi wao.

    Shirika hilo la OECD linatoa jukwaa la kulinganisha uzoefu wa sera,kutafuta suluhu kwa matatizo ya pamoja,kutafuta njia nzuri na kuratibu sera za ndani na za kimataifa za wanachama wake.

    Iwapo itakubaliwa,Rwanda itakuwa nchi ya kwanza ya Afrika kujiunga na shirika hilo.

    Dkt Sezibera alisema Rwanda imetuma ombi la kujiunga na shirika hilo ili kuongeza nguvu kwenye faida kutokana na marekebisho yake ya biashara ,kujifunza na kufanya kazi kwa ukaribu na nchi zilizoendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako