• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yaandikisha punguzo la pengo la biashara

    (GMT+08:00) 2018-11-21 19:50:38

    Rwanda imeshuhudia punguzo la asilimia 36 katika nakisi yake ya biashara tangu mwaka 2015 kutoka na sera ya Made-in-Rwanda ambayo imeongeza uzalishaji wa viwanda katika nchi hiyo.

    Haya yalidokezwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wenye Viwanda nchini Rwanda,Felicien Mutalikanwa,wakati wa sherehe za Siku ya Viwanda Afrika jijini Kigali jana.

    Alisema tangu kuanzishwa kwa sera ya kununua bidhaa za Rwanda mwaka 2015,mauzo ya nje yaliongezeka kwa asilimia 69 kutoka $559 milioni mwaka 2015 hadi $944 milioni mwaka 2017.

    Aidha alibainisha kuwa uagizaji ulipungua kwa asilimia 4,kutoka $1.849 bilioni mwaka 2015 hadi $1.772 bilioni mwaka 2017.

    Kulingana na Mutalikanwa shughuli za utengenezaji bidhaa katika mwaka 2017/18 ziliongezeka kwa asilimia 8 , na kupigwa jeki na shughuli za usindikaji chakula ambazo ziliongezeka kwa asilimia 15.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako