• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Fursa za mafunzo yanayogharamiwa na China zasaidia kupunguza pengo la ujuzi nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2018-11-22 08:54:29

    China imetoa mchango mkubwa kwenye kupunguza pengo la ujuzi nchini Kenya kwa kutoa fursa za mafunzo kwa vijana na watumishi wa umma. Akiongea katika mkutano wa mwisho wa mwaka wa kufanya tathmini ya msaada wa kiufundi wa China kwenye mafunzo na kuendeleza kujenga uwezo, Konsela wa uchumi na biashara wa ubalozi wa China nchini Kenya Bw. Guo Ce, amesema raslimali watu limekuwa ni eneo muhimu kwenye kuhimiza ushirikiano kati ya China na Kenya.

    Amesema karibu watumishi wa umma wapatao elfu 10 wa Kenya wametembelea China na kuhudhuria semina chini ya mpango wa msaada wa mafunzo ulioanzishwa na wizara ya biashara ya China. Bw. Guo amesema China itaendelea kutafuta njia nzuri na zenye ufanisi zaidi ili kuhimiza ushirikiano kati ya China na Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako