• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM - Uchaguzi wa Burundi unatakiwa kuwa huru na wa kuaminika

    (GMT+08:00) 2018-11-22 08:54:49

    Mwenyekiti wa kamati ya kujenga amani ya Umoja wa mataifa Bw. Jurg Lauber, amesema uchaguzi wa Burundi wa mwaka 2020 unatakiwa kuwa shirikishi, wa kidemokrasia na wa amani, na matokeo yake yanatakiwa kukubalika kimataifa. Bw. Lauber amesema tayari uchaguzi huo unafuatiliwa, na utakuwa muhimu kwa mustakbali wa Burundi.

    Bw. Lauber aliyetembelea Burundi mwanzoni mwa mwaka huu amesema Rais Nkurunziza kutangaza kuwa hatagombea urais kwenye uchaguzi ujao, ni hatua muhimu. Ameihimiza serikali na wadau wa kimataifa kujadili ni mambo gani na msaada gani utahitajika ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa mafanikio.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako