• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kuwa mwenyeji wa mkutano wa kikanda kuhusu manunuzi ya umma

    (GMT+08:00) 2018-11-22 08:55:10

    Kenya inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa kikanda kuhusu manunuzi ya umma, kujadili mageuzi ya sasa, mwelekeo na maendeleo yaliyopo kwenye mfumo wa manunuzi ya umma.

    Mkutano huo utakaofanyika kwa siku tatu kuanzia Novemba 28, utawakutanisha washiriki wa sekta binafsi na sekta ya umma, taasisi za kitaaluma, jumuiya za kiraia na taasisi za mafunzo kutoka Burundi, Rwanda, Uganda, Tanzania na wenyeji Kenya.

    Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya usimamizi wa manunuzi ya Umma Bw Maurice Juma, amesema lengo kuu la mkutano huo ni kuwafanya washiriki wajadili mambo yanayoweza kuimarisha usafi, uwazi na uwajibikaji kwenye mifumo ya taifa ya manunuzi ya umma. Bw. Juma amesema washiriki pia wanatarajiwa kujadili matumizi ya Tehama kukabiliana na ufisadi kwenye manunuzi ya umma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako