• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya Afrika mashariki yazindua mfumo wa sera za usalama wa nishati

    (GMT+08:00) 2018-11-22 09:05:21

    Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC imezindua mfumo wa sera za usalama wa nishati unaolenga kutoa mwongozo kwa nchi wanachama kusimamia usalama wa nishati. Akiongea kwenye uzinduzi wa mfumo huo katika mkutano wa kanda ya Afrika mashariki wa Kamisheni ya kiuchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika UNECA uliofanyika mjini Kigali, Rwanda, mtaalamu mwandamizi wa nishati wa EAC Bw. Elsam Byempaka, amesema mfumo huo utazielekeza nchi za Afrika mashariki wakati zinapotekeleza miradi ya nishati kwa ajili ya kupanua upatikanaji wa nishati katika kanda hiyo.

    Ofisa wa UNECA kanda ya Afrika Mashariki Bw. Yohannes Hailu amesema mfumo huo utaboresha ushirikiano wa kikanda kwa ajili ya upatikanaji endelevu na wa uhakika wa nishati ya bei nafuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako