• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanavijiji zaidi ya 1,000 waliokimbia makazi yao kaskazini mwa Msumbiji warudi nyumbani

    (GMT+08:00) 2018-11-22 09:06:08

    Zaidi ya wakazi elfu moja kutoka eneo la Mitumbate, wilaya ya Mocimboa da Praia, kaskazini mwa jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji, wameanza kurudi kwenye vijiji vyao baada ya kukimbia machafuko miezi sita iliyopita, kutokana na mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wasiojulikana ambao walimuua kiongozi wa jamii yao na kuchoma moto nyumba zao.

    Mkuu wa wilaya ya Mocimboa da Praia Bw. Marques Naba amesema wilaya yake imekuwa moja ya maeneo salama zaidi nchini Msumbiji, na familia zimerudi vijijini na kuanza maisha kama kawaida, na vikosi vya usalama bado vinafanya ulinzi kwenye eneo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako