• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika yahitaji kuwa na nia ya kisiasa kufanikisha watu wake kusafiri kwa uhuru

    (GMT+08:00) 2018-11-22 09:34:05

    Maofisa na wataalam wamesema Afrika inahitaji kuwa na nia zaidi ya kisiasa ili kufanikisha watu wake wasafiri kwa uhuru.

    Umoja wa Afrika umesema kuwa nchi 32 za Afrika zimesaini makubaliano kuhusu watu kusafiri kwa uhuru ndani ya bara hilo, haki za ukazi na haki za kujiendeleza barani Afrika. Hata hivyo makubaliano hayo yanahitaji kuidhinishwa kabla ya kuanza kutekelezwa.

    Ofisa wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia mambo ya kijamii Bw. Emelan Leteane, amesema ukosefu wa nia ya kisiasa na uwezo wa nchi za Afrika kutekeleza maamuzi katika ngazi ya mawaziri, umesababisha shida kwa watu kusafiri kwa uhuru barani humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako