• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yahimiza makampuni kuchimba asilimia 70 ya mafuta asili nchini humo

    (GMT+08:00) 2018-11-22 10:06:56

    Sudan Kusini imesema asilimia 70 ya mafuta ya asili nchini humo bado haijachimbwa, na imeyahimiza makampuni ya kimataifa ya nishati kuchimba ili kufufua uchumi wa nchi hiyo.

    Waziri wa mafuta wa Sudan Kusini Bw. Ezekiel Gatkuoth amesema, serikali ya Sudan Kusini imesaini makubaliano ya kuchimba mafuta na makampuni matatu ya kimataifa ya mafuta, ambayo yanalenga kukuza utengenezaji wa mafuta na kutimiza lengo la kunufaishana.

    Bw. Gatkuoth pia amesema ana imani kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu, uchumi wa Sudan Kusini utarudi kwenye kiwango kabla ya vita ya wenyewe kwa wenyewe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako