• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Timu zitakazoshiriki michuano ya mzunguko wa pili kwa vijana U23 zajulikana

    (GMT+08:00) 2018-11-22 10:08:22
    Michuano ya mzunguko wa kwanza, kufuzu kucheza fainali ya bara Afrika katika mchezo wa soka kwa vijana wasiozidi miaka 23 nchini Cairo mwaka ujao, ilimalizika wiki hii na sasa tayari ratiba imeshapangwa kwa michuano ya mzunguko wa pili.

    Baada ya kuishinda Tanzania kwa bao la ugenini, Burundi itamenyana na Congo Brazaville, Kenya itacheza na Sudan, baada ya kufanikiwa kuishinda Mauritius kwa jumla ya mabao 8-1, huku Sudan ikiilemea Ushelisheli kwa jumla ya mabao 2-1.

    DRC nayo itamenyana na Morocco, baada ya kuibamiza Rwanda kwa jumla ya mabao 5-0.

    Ethiopia yenyewe itamenyana na Mali. Mechi hizi, zitachezwa nyumbani na ugenini na mshindi atafuzu latika mzunguko wa tatu na wa mwisho, ili kutafuta timu nane bora kutafuta ubingwa wa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako