• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • AWCON: Timu ya wanawake ya Mali yaiburuza Ghana kwa mabao 2-1

  (GMT+08:00) 2018-11-22 10:10:32

  Timu ya taifa ya mchezo wa soka ya Mali, kwa upande wa wanawake, imefufua matumaini ya kusonga mbele katika hatua ya mtoano kuwania taji la bara Afrika baada ya kuwafunga wenyeji Ghana mabao 2-1 katika mechi yake ya pili Juzi jijini Accra.

  Mechi ya kwanza, Mali ilianza vibaya baada ya kufungwa na Cameroon mabao 2-1. Hata hivyo, Cameroon itandeleza ushindi katika mechi ya kundi A baada ya kushinda Algeria mabao 3-0.

  Kwa matokeo haya, Cameroon wanaongoza kundi hilo kwa alama sita, Mali ni ya pili kwa alama tatu sawa na Ghana, huku Algeria ikiwa ya mwisho bila alama.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako