• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Barcelona yakatwa ngebe kuibomoa Liverpool hadi 2021

    (GMT+08:00) 2018-11-22 10:10:21
    Klabu ya Barcelona imejikuta njia panda baada ya kukatwa ngebe za usajili wa dirisha dogo endapo itamtaka mchezaji wa klabu ya Liverpool.

    Mabingwa hao wa ligi kuu ya Uhispania, wametakiwa kukaa miaka 3 bila kusajili nyota yeyote wa Liverpool.

    Kwa mujibu wa makubaliano ya klabu hizo, Barcelona haitasajili mchezaji wa Liverpool hadi mwaka 2021. Taarifa hiyo imetolewa wakati mshambuliaji nyota wa Liverpool Mo Salah akihusishwa na mpango wa kujiunga na Barca katikia usajili wa dirisha dogo Januari mwakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako