• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Urefu wa barabara za vijijini nchini China wazidi kilomita milioni 4

  (GMT+08:00) 2018-11-22 17:55:16

  Hivi karibuni wizara ya mawasiliano na uchukuzi ya China imetoa kanuni za usimamizi zinazolenga kutatua masuala makubwa ya usimamizi wa ujenzi wa barabara za vijijini, na kuthibitisha zaidi utaratibu wa wajibu wa maisha kuhusu ubora wa barabara za vijijini. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2017, urefu wa barabara za vijijini ulikuwa umefikia kilomita milioni 4.01, ambao unachukua asilimia 84 ya urefu wa barabara zote nchini China.

  Akiongea kuhusu hali ya uwepo wa barabara, Msemaji wa wizara ya mawasiliano na uchukuzi ya China Bw. Wu Chungeng amesema bado kuna matatizo kadhaa kwenye ujenzi wa barabara vijijini, akisema,

  "Miradi ya ujenzi wa barabara vijijini ni mingi na midogo, na iko katika sehemu mbalimbali. Miradi hiyo bado ina matatizo kadhaa, ikiwemo usimamizi duni wa ujenzi, uwezo mdogo wa kusimamia ubora na ukosefu wa watu wanaowajibika, ambayo yamezuia ubora wa barabara vijijini usiinuliwe kikamilifu."

  Katika hali hiyo, wizara hiyo ilitoa kanuni za usimamizi wa ubora wa ujenzi wa barabara vijijini. Msemaji huyo amesema,

  "Kanuni hizi zimethibitisha utaratibu wa wajibu wa maisha kuhusu ubora wa barabara za vijijini, zimeamua kujenga utaratibu wa kikazi wa kusimamia ubora wa ujenzi wa barabara kwa uratibu, kati ya idara za ngazi mbalimbali na udhibiti wenye ufanisi mkubwa wa pande zote, na zimesisitiza kudhibiti mambo nane yakiwemo usanifu, raslimali za ujenzi, ukaguzi wa ubora wa ujenzi na sifa ya makampuni".

  Kanuni hizi zinasema ifikapo mwaka 2020, ubora wa barabara za vijijini na uhakikisho wa usalama wake vitaboreshwa, miradi itadumu zaidi na itakuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kukabiliana na maafa, na utaratibu wa usimamizi wa ubora wa barabara utaimarika zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako