• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lataka uchaguzi mkuu wa DRC kufanyika kwa mafanikio

    (GMT+08:00) 2018-11-22 18:11:41

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesema uchaguzi mkuu utakaofanyika Desemba 23 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ni muhimu sana kwa nchi hiyo na kuzitaka pande mbalimbali kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa mafanikio.

    Taarifa iliyotolewa na Baraza hilo imesisitiza kuwa, uchaguzi huo utatoa fursa ya kihistoria kwa nchi hiyo kutimiza kwa mara ya kwanza kukabidhi mamlaka kwa amani, kuimarisha utulivu wa jamii na kuendeleza uchumi. Pia Baraza hilo limevitaka vyama vyote vya siasa, wafuasi wao na wanasiasa wengine kufuata kwa pande zote katiba, makubaliano husika ya kisiasa na ratiba ya uchaguzi mkuu, na kushiriki mchakato wa uchanguzi kwa amani, ili kuhakikisha uwazi, utulivu, uaminifu wa uchaguzi na kulinda amani na utulivu wa nchi hiyo na ukanda huo.

    Aidha, taarifa hiyo imezihimiza pande mbalimbali kutotumia mabavu, kudumisha kiwango cha juu zaidi cha kujizuia, kuepusha vitendo vya uchochezi na kutatua migongano kwa njia ya amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako