• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yalihimiza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuondoa Burundi kutoka ajenda za Umoja huo

    (GMT+08:00) 2018-11-22 18:52:47

    Naibu balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao amesema hali ya sasa ya Burundi ni imara, Baraza la Usalama linapaswa kusikiliza sauti ya Burundi na kufikiria kuondoa nchi hiyo kutoka ajenda za umoja huo.

    Bw. Wu amesema hayo katika mjadala wa wazi wa Baraza la Usalama juu ya suala la Burundi, ameongeza kuwa serikali ya Burundi imetekeleza kikamilifu mchakato wa kisiasa na kupata maendeleo muhimu na idadi kubwa ya wakimbizi wamerudi nyumbani kwao. Pia amesema mwelekeo wa upatanisho , mshikamano wa kijamii na ushirikiano wa kisiasa umeendelea kuimarishwa nchini humo, ikiwa ni ishara kuwa serikali ya Burundi na wananchi wake wana uwezo na nia ya kutatua masuala ya kisiasa ya ndani na kulinda amani na utulivu wa kitaifa kwa kujitegemea.

    Amesema serikali ya China siku zote inaunga mkono mchakato wa amani wa Burundi na imetoa msaada kwa ukarabati wa nchi hiyo, na kwamba China inapenda kuendelea kutoa mchango wa kiujenzi kwa kutimiza amani, utulivu na maendeleo endelevu nchini Burundi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako