• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WTO yakubali kuanzisha timu ya wataalamu kutathmini nyongeza ya ushuru wa chuma cha pua na alumini iliyotolewa na Marekani

    (GMT+08:00) 2018-11-22 18:53:06

    Idara inayoshughulika na utatuzi wa mikwaruzano ya kibiashara ya Shirika la Biashara Duniani (WTO) imekutana na kukubali kuanzisha timu ya wataalamu itakayotathmini nyongeza ya ushuru wa chuma na alumini iliyotolewa na Marekani mwezi Marchi.

    Hatua hiyo imetokana na maombi yaliyotolewa na China, Umoja wa Ulaya, Canada, Mexico, Norway, Russia na Uturuki, ili kutathimini kama hatua ya Marekani inakwenda kinyume na kanuni za Shirika hilo.

    Kwenye mkutano huo, wajumbe 7 wamesema hatua ya Marekani ni ya kujilinda na lengo lake ni kulinda chuma cha pua na alumini za Marekani zisiathiriwe na bidhaa zinazoingizwa kutoka nje, hatua ambayo inakisiwa kwenda kinyume na kanuni za WTO.

    Aidha kwenye mkutano huo India na Uswisi zimetoa maombi yao ya kwanza ya kuanzisha timu ya kutathmini ushuru ya Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako