• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yachunguza chanzo cha vifo vya faru watatu

    (GMT+08:00) 2018-11-22 18:57:02

    Mamlaka ya wanyamapori nchini Kenya imethibitisha vifo vya faru watatu weusi vilivyotokea katika Hifadhi ya Taifa ya Masai Mara iliyoko kaskazini magharibi mwa nchi hiyo, na kusema uchunguzi unaendelea kujua chanzo cha vifo hivyo.

    Shirika la Huduma ya Wanyamapori la Kenya limesema, faru hao, wawili wakubwa na mmoja mdogo, walikutwa wamekufa katika matukio tofauti ndani ya wiki mbili, na kusema madaktari wa mifugo wanafanyia vipimo mizoga hiyo ili kugundua sababu halisi ya vifo vyao.

    Shirika hilo limesema mizoga ya faru hao iliripotiwa kati ya tarehe 12 na 19 mwezi huu na wahifadhi kutoka Mara Triangle wakati wakifanya doria ya kawaida katika hifadhi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako