• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini: Kampuni ya mafuta ya Russia kutafuta mafuta Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2018-11-22 18:59:39

    Kampuni ya mafuta ya Russia Gazprom Neft imesaini mkataba wa maelewano na serikali ya Sudan Kusini ili kufanya utafutaji wa mafuta nchini humo.

    Waziri wa Petroli wa Sudan Kusini Ezekiel Lol Gatkuoth amesema kampuni hiyo itafanya utafiti kwenye maeneo manne.

    Waziri huyo amesema uzalishaji wa mafuta nchini humo umeongezeka khadi mapipa 135,000 kwa siku kutoka mapipa 130,000 ya mwezi Agosti.

    Amesema nchi hiyo inalenga kurejesha uzalishaji wa hadi mapipa 350,000 kwa siku kama ilivyokuwa mwaka 2011 wakati ilipojitenga na Sudan.

    Kampiuni nyingine ambazo zimewekeza kwenye sekta ya mafuta nchini humo ni pamoja na CNPC ya China na Petronas ya Malaysia .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako