• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Kampuni ya Emerson yatoa mafunzo Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-11-22 19:00:00

    Kampuni ya Emerson inayotengeneza mitambo na vipuri duniani imetoa mafunzo bure yatakayosaidia wadau kutoka taasisi mbalimbali, kuongeza ujuzi katika mashine za kupima viwango na ubora wa mafuta na gesi nchini maarufu flow meters.

    Kampuni hiyo kwa kushirikiana na kampuni ya Petrogas wametoa mafunzo hayo jijini Dar es Salaam kwa washiriki 52 waliowakilisha kampuni binafsi na umma nchini.

    Mafunzo hayo yamejikita katika mita mbili zinazotengenezwa na kampuni ya Emerson, ambazo ni Micro Motion Coriolis Flow Meters zenye umbo la herufi U na Daniel Ultra Sonic Flow Meters.

    Kiongozi wa jopo la watalaamu wa kampuni ya Emerson kutoka nchini Marekani, William Fernandes amesema faida za mafunzo hayo ya siku moja kwa Tanzania iliyojikita kwenye uchumi wa viwanda, yataongeza uwezo wa kutambua ubora wa bidhaa hizo katika masoko ya nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako