• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Jukwaa la fursa za biashara na uwekezaji laanzishwa Tabora

    (GMT+08:00) 2018-11-22 19:00:17

    Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda wa Tanzania ameupongeza mkoa wa Tabora kwa kuaandaa jukwaa la fursa za biashara na uwekezaji.

    Amesema mkoa huo umefanya jambo zuri la kuandaa jukwaa hilo ambalo matunda yake yataunufaisha mkoa na taifa kwa ujumla.

    Waziri Kakunda amesema kwa kujua umuhimu wa jukwaa hilo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ndiye atakayelizindua.

    Wakati huohuo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri kwa niaba ya wakazi wa mkoa wa Tabora amempongeza Kakunda ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Sikonge kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako