• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia : Eagle Hills, yazindua mradi wa dola bilioni 2 Addis Ababa

    (GMT+08:00) 2018-11-22 19:00:37

    Kampuni moja ya Abu Dhabi, Eagle Hills, imezindua mradi wa dola bilioni 2 wa kujenga makaazi ya kisasa mjini Addis Ababa, Ethiopia.

    Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema serikali itakuwa na mgao wa asilimia 27 kwenye mradi huo ambao unajumuisha maduka, nyumba 4,000 na hoteli tatu za ngazi ya nyota tatu.

    Mradi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya miaka saba na zaidi ya familia 1,600 zinazoishi kwenye eneo la mradi zitapata nyumba mpya.

    Aidha mradi huo utafungua fursa 25,000 za ajira nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako