• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa nne wa mawaziri wakuu wa China na Kazakhstan wafanyika

    (GMT+08:00) 2018-11-22 20:46:15

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang na mwenzake wa Kazakhstan Bw. Bakytzhan Sagintayev wamefanya mkutano wa nne wa mawaziri wakuu wa nchi hizo mbili katika jumba la mikutano hapa Beijing leo mchana.

    Bw. Li Keqiang amesema, China inapenda kushirikisha pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" na mkakati wa maendeleo ya Kazakhstan, ili kugeuza matarajio ya kuaminiana na kushirikiana kati ya pande mbili kuwa mafanikio halisi na kuwanufaisha watu wao.

    Bw. Sagintayev amesema, Kazakhstan inapenda kushirikisha mpango wa "Nurly Zhol" na pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", kuimarisha ushirikiano katika sekta za biashara, uwekezaji, uzalishaji, kilimo na nishati. Pia kuimarisha mafunzo yanayotolewa kwa wafanyakazi na kubadilishana uzoefu, ili kusukuma mbele uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako