• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: AWCON 2018: Nigeria yafufua matumaini baada ya kutoa dozi

    (GMT+08:00) 2018-11-23 08:10:21
    Mabingwa watetezi wa kombe la ubingwa la bara Afrika katika mchezo wa soka kwa upande wa wanawake (AWCON) Super Falcons ya Nigeria, hatimaye wamefufua matumaini ya kusonga mbele katika fainali za mwaka huu zinazoendelea jijini Accra nchini Ghana, baada ya kuifunga Zambia mabao 4-0 katika mechi yake ya pili.

    mambo yanaendelea kuwa mabaya kwa Equitorial Guinea ambao walipoteza mechi yake ya pili baada ya Afrika Kusini kupata karamu ya mabao 7-1.

    Baada ya matokeo hayo, Afrika Kusini inaongoza kundi la B, kwa alama 6, huku Nigeria na Zambia zikiwa na alama tatu.

    Leo Ijumaa kutakuwa na michuano ya kumaliza kundi A, Cameroon watachuana na Ghana, huku Algeria wakicheza na Mali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako