• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RAGA: Mabadiliko kikosini Simbas duru za Dubai na Cape Town zikinukia

    (GMT+08:00) 2018-11-23 08:11:17
    Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Raga ya wachezaji 7 kila upande ya Kenya(Simbas) Paul Murunga, amefanya mabadiliko sita ikiwemo kujumuisha sura mpya Daniel Taabu, Johnston Olindi na Brian Wahinya katika kikosi kitakachowania ubingwa wa duru mbili za ufunguzi za mchezo wa raga ya dunia msimu 2018/2019 katika miji ya Dubai na Cape Town -Afrika Kusini.

    Duru za Dubai na Cape Town zitakuwa mtihani mzuri kwa Kenya kuona kama inapiga hatua mbele katika kuunda kikosi kipya ama bado inahitaji wachezaji wengi walio na uzoefu ambao imewacha nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako