• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Didier Drogba atundika daluga baada ya viwanjani kwa miaka 20

  (GMT+08:00) 2018-11-23 08:12:39

  Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa timu ya taifa ya soka ya Cote d'Ivoire Didier Drogba, amesema anatundika daluga, baada ya zaidi ya miaka 20 katika viwanja vya mchezo wa soka.

  Drogba mwenye umri wa miaka 40, anastaafia katika klabu ya Phoenix Rising nchini Marekani.

  Alianza kucheza ya kulipwa mwaka 1998 katika klabu ya Le Mans nchini Ufaransa, kabla ya kwenda katika klabu ya Guingamp na baadaye kwenda Marseille.

  Hata hivyo, umaarufu wake ulifahamika sana katika klabu ya Chelsea nchini Uingereza, alikofunga mabao 164 katika mechi 341.

  Aliichezea timu yake ya taifa kati ya mwaka 2002-2014 na kuichezea mechi 104 na kufunga magoli 65, rekodi ambayo bado anaishikilia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako