• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yatengeneza mbegu za ndizi zinazohimili magonjwa na ukame

    (GMT+08:00) 2018-11-23 08:58:57

    Taasisi ya utafiti wa kilimo ya Tanzania TARI imetangaza kuwa imetengeneza aina 16 za mbegu za ndizi zinazoweza kuhimili ukame na magonjwa, na kutarajiwa kuleta mapinduzi ya kilimo Tanzania.

    Mtafiti wa kituo cha utafiti cha TARI Uyole Mbeya Bw Daudi Mbongo, amesema aina hizo zimetengenezwa na watafiti wenyeji katika mikoa mitatu inayozalisha ndizi ya Mbeya, Kilimanjaro na Kagera. Pia amesema aina hizo 16 zinatoa mazao mengi kuliko aina nyingine za kawaida.

    Mtafiti mwingine kituo cha TARI-Uyole Bw. Tulole Buchyeyeki, amesema aina hizo mpya ni ahueni kubwa kwa wakulima, kwa kuwa zimethibitisha kuwa na mazao mengi, zinahimili magonjwa na kuvumilia ukame.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako