• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika Mashariki kuoanisha TEHAMA kuvutia uwekezaji toka nje

    (GMT+08:00) 2018-11-23 08:59:17

    Nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki zinapanga kuoanisha sekta ya Tehama, ili kuvutia uwekezaji zaidi wa moja kwa moja kutoka nje.

    Mkurugenzi wa Mamlaka ya mawasiliano ya Kenya Bw. Francis Wangusi amewaambia wanahabari mjini Nairobi kuwa nchi sita wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki zina masoko madogo madogo ambayo yana ukomo kwenye kuvutia uwekezaji kutoka nje.

    Bw. Wangusi amesema kwa sasa nchi za Afrika Mashariki zina sheria tofauti za kusimamia sekta ya Tehama. Watalaam kutoka nchi zote wanachama wameanza kuandaa rasimu ya sheria zitakazoweza kutekelezwa kwenye nchi zote wanachama. Hatua hiyo ina lengo la kuoanisha sheria zote za Tehama kwenye eneo hilo na kuunda soko kubwa lenye watu milioni 160.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako