• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 143 wathibitishwa kufariki kutokana na homa ya Lassa Nigeria

    (GMT+08:00) 2018-11-23 09:01:11

    Nigeria imethibitisha kuwa watu 143 wamefariki dunia kutokana na homa ya Lassa nchini humo kwa mwaka huu. Kwa mujibu wa Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa cha Nigeria NCDC, kuanzia mwezi Januari hadi Novemba, watu 3,016 walioshukiwa kuambukizwa homa ya Lassa katika majimbo 22 na kata 90 wameripotiwa, kati yao watu 559 wamethibitishwa.

    Msemaji wa NCDC Bw. Chimezie Anueyiagu amesema mjini Abuja kuwa kiwango cha vifo kutokana na homa hiyo mpaka sasa kimethibitishwa kuwa ni asilimia 22.6, na kwamba Nigeria imekuwa na mipango ya kupitia miongozo iliyopo sasa, na kuweka mkakati wa miaka mitano ili kupambana na homa ya Lassa. Imefahamika kuwa mwaka huu maambukizi ya homa ya Lassa pia yameripotiwa nchini Ghana, Benin, Liberia na Sierra Leone.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako