• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Somalia yaunga mkono ufumbuzi wa ITU kuhusu msaada maalum

    (GMT+08:00) 2018-11-23 09:01:48

    Serikali ya Somalia imekaribisha kupitishwa kwa ufumbuzi kwenye Umoja wa Mawasiliano ya Simu wa Kimataifa ITU, ambao utakuwa na athari ya moja kwa moja na kuhusiana na maslahi maalumu ya nchi hiyo.

    Waziri wa posta, mawasiliano ya simu na teknolojia wa Somalia Bw. Abdi Ashur Hassan amesema lengo la Azimio 34 ni kutoa ufuatiliaji maalum kwa Somalia kutokana na mgogoro uliodumu wa muda mrefu nchini humo na kutoa msaada na uungaji mkono katika kujenga upya miundombinu ya mawasiliano ya simu nchini Somalia.

    Mkutano mkuu wa 20 wa Umoja wa mawasiliano ya simu wa kimataifa ITU ulifungwa Ijumaa iliyopita nchini UAE, ambapo nchi wanachama wamesisitiza tena ahadi zao kwa Ruwaza ya pamoja ya kujenga dunia inayoungana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako